Mwingiliano wa Ufundishaji, Lugha ya Kiswahili na Mazingira ya Ujifunzaji katika Kujenga Umahiri wa Lugha na Maarifa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi nchini Tanzania

Authors

  • Steven Yesaya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, Tanzania Author

DOI:

https://doi.org/10.33687/ijef.003.03.00142

Keywords:

Kiswahili, lugha ya kufundishia, mazingira ya ujifunzaji, umahiri wa lugha, maarifa, elimu ya msingi, Tanzania

Abstract

Makala hii inachunguza nafasi ya mwingiliano wa ufundishaji, matumizi ya lugha ya Kiswahili na mazingira ya ujifunzaji katika kujenga umahiri wa lugha na maarifa kwa wanafunzi wa shule za msingi nchini Tanzania. Lengo kuu la makala ni kubainisha namna lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia inavyoathiri uelewa wa wanafunzi katika masomo mbalimbali pamoja na ushiriki wao katika mchakato wa ujifunzaji darasani. Utafiti wa Makala hii umeongozwa na nadharia ya Ujenzi wa Maarifa ya Lev Vygotsky, inayosisitiza kuwa lugha ni nyenzo muhimu ya kujenga fikra, maarifa na kukuza ujifunzaji wa mwanafunzi kupitia mwingiliano wa kijamii. Mbinu za utafiti zilizotumika ni uchambuzi wa nyaraka, mahojiano, pamoja na uchunguzi. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa matumizi ya Kiswahili katika ufundishaji huchochea uelewa wa dhana za kitaaluma kwa wanafunzi wa shule za msingi, huimarisha ushiriki wa wanafunzi darasani na kukuza uwezo wa kufikiri kwa kina. Hata hivyo, utafiti umebaini kuwa bado kuna changamoto zinazohusiana na uhaba wa nyenzo za kufundishia na kujifunzia pamoja na mitazamo hasi ya kijamii kuhusu nafasi ya Kiswahili kama lugha ya maarifa. Makala inapendekeza kuimarishwa kwa sera ya lugha ya kufundishia, kuendelezwa kwa istilahi za kitaaluma za Kiswahili, pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya ujifunzaji ili kuongeza ufanisi wa elimu ya msingi nchini Tanzania. Utafiti unahitimisha kuwa Kiswahili kina nafasi muhimu katika kujenga msingi wa umahiri wa lugha na maarifa kwa wanafunzi na hivyo kuchangia kuboresha ubora wa elimu nchini.

Downloads

Published

2026-07-21

Issue

Section

Research Articles

How to Cite

Mwingiliano wa Ufundishaji, Lugha ya Kiswahili na Mazingira ya Ujifunzaji katika Kujenga Umahiri wa Lugha na Maarifa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi nchini Tanzania (S. Yesaya , Trans.). (2026). International Journal of Education Foundations, 3(3), 565-572. https://doi.org/10.33687/ijef.003.03.00142

Similar Articles

11-20 of 127

You may also start an advanced similarity search for this article.