Sauti za Ziwani: Uchambuzi wa Nyimbo za Uvuvi za Kisukuma kama Chombo cha Mawasiliano ya Jamii katika Mwambao wa Ziwa Victoria
DOI:
https://doi.org/10.33687/ijef.003.03.00141Keywords:
Nyimbo za uvuvi, Wasukuma, mawasiliano ya jamii, fasihi simulizi, Nadharia ya UamilifuAbstract
Makala hii inachunguza mchango wa nyimbo za uvuvi za Kisukuma kama chombo cha mawasiliano ya jamii na maendeleo ya kijamii miongoni mwa wavuvi wa mwambao wa Ziwa Victoria. Utafiti umeongozwa na Nadharia ya Uamilifu iliyoasisiwa na Bronislaw Malinowski, A.R. Radcliffe-Brown na Franz Boas. Data zilikusanywa kupitia usaili na ushuhudiaji shirikishi miongoni mwa wavuvi wa jamii ya Wasukuma katika Mkoa wa Mwanza. Matokeo yanaonesha kuwa nyimbo za uvuvi hutumika kuhamasisha uwajibikaji, kuimarisha mshikamano, kueleza hisia mbalimbali na kutoa tahadhari kuhusu hatari zinazoweza kujitokeza ziwani. Aidha, nyimbo hizi huchangia katika kuhifadhi maarifa ya jadi na kuendeleza maadili ya kazi. Makala inahitimisha kuwa nyimbo za uvuvi za Kisukuma ni zaidi ya burudani; ni nyenzo muhimu ya mawasiliano na urithi wa kitamaduni unaostahili kuhifadhiwa na kuendelezwa.
Downloads
Published
Issue
Section
License
Copyright (c) 2026 Steven Yesaya (Author)

This work is licensed under a Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International License.




